TAARIFA: Wachezaji wa Simba watakao ukosa mchezo wa Power Dynamos ligi ya Mabingwa


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji watatu wataukosa mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos


Mchezo huo utapigwa Jumapili, Oktoba 1 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi


Ahmed amesema beki Hennock Inonga bado anaendelea kuuguza jeraha alilopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji


Ahmed pia amewataja mlinda lango Aishi Manula ambaye bado anaendelea kuimarika wakati Aubin Kramo hayuko tayari kutumika kwenye mechi ya ushindani kwani kuwa bado hajapona sawasawa majeraha


"Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki timu ilirejea mazoezini jana kujiandaa na mchezo dhidi ya Power Dynamos"


"Mpaka sasa ni wachezaji watatu (Inonga, Kramo, Manula) ambao tuna uhakika wataukosa mchezo lakini wachezaji wengine wote wanaendelea na maandalizi"


"Tunatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki ili kuwaweka sawa wachezaji kuelekea mchezo husika. Ni takribani siku 9 wachezaji hawatakuwa na mechi yoyote kitaalamu hili sio jambo zuri kuelekea mchezo muhimu ambao tunahitaji matokeo mazuri ili kutinga hatua ya makundi," alisema Ahmed

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post