Skudu akiri mambo magumu Yanga "Sio rahisi kupata namba"

Skudu Makudubela.

 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Winga wa Klabu ya Yanga, Skudu Makudubela amesema kuwa mara baada ya kutoka kwenye majeraha, sasa amerejea kwenye mazoezi na yupo fiti hivyo anasubiri mwalimu Miguel Gamondi kumpa majukumu.


Skudu amesema hayo mara baada ya kurejea nchini na kikosi cha Yanga kikitokea Rwanda kwenye mchezo wao wa ligi ya Mabingwa Afrika ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya wenyeji wao Al-Merrikh ya Sudan.


Skudu ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Marumo Gallants aliumia dakika ya 6 ya mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya jamii hdidi ya Azam FC katika Dimba la Mkwakwani na kulazimika kupewa ruhusa ya kwenda kwao Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kabla ya kurejea tena wiki kadhaa zilizopita na kuungana na wenzake.


"Nimetoka kwenye majeraha yaliyokuwa yameniweka nje na nimepona kabisa na nimekuwa nikifanya kazi kubwa uwanja wa mazoezi kurejesha kiwango changu na kumshawishi mwalimu.


"Ukweli ni kwamba timu yetu inafanya vyema na ninafurahia sana na nyie nadhani mnaona. Hivyo kiukweli inahitaji kujituma zaidi na kufanya kazi kwa nguvu kwa maana sio rahisi kuingia kwenye kikosi, kila mchezaji anafanya vyema.


"Watu wawe na subira muda ukifika wataniona uwanjani mwalimu akiridhika na urejeo wangu na utimamu wangu basi mtaniona tena uwanjani na muda ukifika kazi itafanywa kweli kweli.


"Mwisho kabisa niwaombe mashabiki wajitokeze tena Chamazi kwenye michezo yetu mingine hata ule wa marudiano tutakapoenda kumaliza kazi dhidi ya Al-Merreick, kujituma kwetu kunachagizwa na wao," amesema Skudu

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post