Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema Simba itapita mashuleni kwa ajili ya kutafuta mashabiki wapya pamoja na kusaka vipaji vipya vya wachezaji ambao watawaendeleza
Mkuu wa Programu za vijana, Patrick Rweyemamu amepewa jukumu la kusimamia mchakato huo katika mashule
Katika sehemu ya mpango huo, Kajula amesema kwenye mechi zake Simba itatoa mialiko kwa shule mbalimbali ili kuwapa fursa watoto kujifunza na kwendana na utamaduni wa Simba tangu utotoni
Mpango huo utafanyika sambamba kwa ushirikiano na Washirika wa Simba benki za CRDB na NMB. Benki hizo zimeandaa kadi maalum zinazojulikana kama Simba Caps (Mtoto wa Simba)
"Tumezindua Programu maalum tuliyoipa jina la Back to School kwa ajili ya kutembelea shule mbalimbali nchi nzima ili kuandaa mashabiki wapya pamoja na kuvumbua vipaji kwakuwa makocha wetu watakuwa wanatembelea huko," alisema Kajula
Post a Comment