Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Simba SC, imesema iwe mvua iwe jua, lazima iwashushie kichapo Power Dynamos katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa Jumapili, Oktoba 1, 2023 katika Uwanja wa Azam Comlex-Chamazi jijini Dar.
Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo utakaoamua hatima yao ya kwenda makundi baada ya ule wa awali kumalizika kwa sare ya 2-2 huko Zambia.
"Tarehe moja ya mwezi wa kumi ni siku ya Mnyama kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Sisi hatwendi kuweka historia, tunakwenda kwenye miasha yetu ya kawaida."
"Tunafahamu mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, wote mliona namna walivyotusumbua lakini wanakuja nyumbani Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama na hicho hicho atakutana nacho. Bora wangekubali tukamalizana nao kwao," alisem Ahmed.
Post a Comment