Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira ametaka mechi moja ya kirafiki kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos ambao utapigwa Jumapili, Oktoba 1 katika uwanja wa Azam Complex
Simba imerejea mazoezini leo kuendelea na maandalizi ya mchezo huo baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki
Imeelezwa Simba huenda ikachuana na Pan African katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Mo Simba Arena, siku ya Jumanne, saa 3 asubuhi
Mwishoni mwa wiki hakukuwa na mechi za ligi kuu ya NBC, ligi ikiwa imesimama kwa wiki mbili ambapo Bodi ya ligi imetoa ufafanuzi uwepo wa kalenda ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani
Hata hivyo hakuna ratiba yoyote iliyotolewa na CAF kuhusu michuano hiyo licha ya TFF kudai kuiandikia barua CAF mapema ili kupata uthibitisho kama ipo au la
Post a Comment