Sibomana awakaribisha Wananchi Rwanda


 Winga wa zamani wa Yanga Patrick Sibomana 'PS Machine' amewakaribisha Wananchi nchini Rwanda katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh


Sibomana ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Gor Mahia ya Kenya, bado ni Mwananchi kindakindaki


Aliitumikia Yanga kwa misimu miwili 2018-19 kabla ya kurejea Rwanda kuitumikia AS Kigali


"Nawakaribisha Wanayanga mje kwa wingi Rwanda ili tuishangilie timu yetu iweze kupata ushindi," alisema Sibomana


Mpaka sasa mabasi manne ya kubeba mashabiki kuwapeleka Rwanda yamejaa, ni wazi Jiji la Kigali litapambwa kwa rangi ya njano na kijani siku ya Jumamosi Septemba 16

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post