Robertinho awekwa kati na mashabiki

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Pamoja na kuwa Simba bado haijafanya vibaya chini ya kocha Robertinho Oliveira lakini presha imeanza kuwa kubwa mashabiki wakionyeshwa kutoridhishwa na mbinu zake


Msimu huu Robertinho ameiongoza Simba kushinda Ngao ya Jamii mkoani Tanga na pia ameshinda mechi mbili za ligi kuu ambazo Simba imecheza mpaka sasa


Mchezo wake wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga makundi ligi ya mabingwa ukamalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2 ugenini nchini Zambia


Hayakuwa matokeo mabaya kwa Simba hasa ikizingatiwa mchezo huo umechezwa ugenini lakini ambacho hakikuwafurahisha mashabiki ni kiwango kilicho-onyeshwa na timu yao hasa kwenye kpindi cha kwanza


Msimu uliopita Simba ilikuwa na kikosi finyu, msimu huu mambo ni tofauti, kikosi kimekamilika hivyo ni wazi timu inapokuwa haifanyi vizuri lawama zinakwenda kwa kocha na benchi lake la ufundi


Hofu ya baadhi ya mashabiki ni kuwa pengine Robertinho hawatumii wachezaji wake alionao ipasavyo, lakini mwisho wa siku yeye ndio kocha, anajua amtumie mchezaji gani katika mbinu zake


Ni wazi Robertinho sasa anaweza kuwa kwenye wakati mgumu kwani anapaswa kuhakikisha Simba inashinda mchezo unaofuta kwenye ligi kuu na pia kuhakikisha Simba inatinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa


Kama Simba itakosa ushindi katika moja ya mechi hizi mbili zinazofuata, presha itakuwa kubwa zaidi kwake na inaweza kwenda kuamua hatma yake


Simba imejiwekea malengo msimu huu, inataka kurejesha mataji yote ya ndani waliyopoteza kwa misimu miwili lakini pia angalau kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika


Hofu ya Wanasimba iko huku kwenye michuano ya Kimataifa, lakini mpaka sasa tunaweza kusema bado Robertinho yuko kwenye njia sahihi kwa sababu timu yake haijafanya vibaya

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post