Robertinho aweka mikakati sawa ya Ushindi Zambia


Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia


Mchezo huo utapigwa Septemba 16 katika uwanja wa Levy Mwanawasa huko Zambia na mchezo wa marudiano kupigwa wiki mbili baadae katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam


Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema anakiandaa kikosi chake kimbinu ili kuhakikisha wanakwenda kupata matokeo mazuri ugenini ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga makundi


"Maandalizi ya mchezo dhidi ya Power Dynamos tulianza mapema, tunajiandaa kimbinu ili kuhakikisha tunakwenda kupata matokeo mazuri ugenini na nyumbani katika mechi ya marudiano"


"Wachezaji wanafahamu nini wanapaswa kufanya tunapocheza ugenini na nyumbani. Jambo muhimu lazima tucheze kitimu tukiwa na mpira na hata bila ya mpira, tutumie vyema nafasi tunazotengeneza kuhakikisha tunafunga magoli ugenini"


"Tuna timu nzuri yenye wachezaji wenye uzoefu mkubwa na mashindano haya, nafikiri tutakuwa katika ubora na kuweza kupata matokeo ya ushindi na kuingia hatua ya makundi," alisema Robertinho


Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kipanga Fc katika mchezo wa kirafiki, Simba inatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki kabla ya kuelekea Zambia

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post