Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefanya kazi ya ziada ya kukutana na mchezaji mmoja mmoja ili kufanikisha mipango ya kushinda mchezo wa Mkondo wa Pili wa kuwania Kufuzu Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, dhidi ya Power Dynamos.
Simba SC itarudiana na Dynamos Jumapili (Oktoba Mosi) katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam, baada ya awali kutoka sare ya mabao 2-2 ugenini mjini Ndola, Zambia.
Robertinho amekuwa akidili na mchezaji mmoja moja akianza na wale wanaocheza eneo hilo la ulinzi akiwapanga jinsi gani ya kucheza kwa utulivu kwenye mchezo huo.
Mbali na mabeki, pia Robertinho amefanya vikao kama hivyo na wachezaji wanaocheza eneo la kiungo lakini pia wale wanaocheza mbele akijifungia na mchezaji mmoja mmoja.
Kocha Robertinho amesema nafasi kubwa imekuwa ni kuwatengeneza kisaikolojia wachezaji wa timu hiyo, huku akiwakumbusha pia juu ya ubora wa wapinzani hao waliotoka nao sare awali.
Robertinho amesema wanahitajika kucheza kwa nidhamu kubwa eneo la ulinzi ili kuhakikisha hawaruhusu mabao ambayo yatawatibulia hesabu zao lakini pia kuwa imara kwenye eneo la kiungo ambalo litatumika kutuliza ukuta wao na kutengeneza nafasi za mabao.
“Mabao mawili tuliyoyapata kule ugenini yatatusaidia hapa na wao yaliwaumiza lakini tunaporudi nyumbani hatutakiwi kuzubaa.” amesema Robertinho
Chanzo: Dar24
Post a Comment