Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Yanga Sc Injinia Hersi Said amewanunulia tiketi mashabiki wote wa timu hiyo waliosafiri na timu Rwanda kwa ajili ya mchezo dhidi ya Al Merreikh
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi saa 9 Alasiri (saa 10 Tanzania) katika uwanja wa Pele, Kigali Rwnada
Akizungumza na mashabiki hao nje ya uwanja wa Pele zamani Nyamirambo, Hersi amesema ni heshima kubwa kwa Yanga kuwa na mashabiki ambao wako tayari kujitoa kwa timu yao
Pamoja ya kuwashukuru kwa kusafiri kwa wingi, Hersi alisema wote watapatiwa tiketi zao bure ili waweze kushuhudia mchezo huo
"Sitakuwa na fadhila kama mmesafiri umbali mrefu kuifuata timu kisha mkalipa viingilio, namuagiza Mfikirwa kulisimamia zoezi lenu kuhusu tiketi, hivyo ‘suala la tiketi kesho ondoeni shaka" alisema Hersi
Kiingilio cha chini katika mchezo huo ni Tsh 21,000/-. VIP ni Tsh 104,000/-, Daraja la kati ni Tsh 52,000/- na Kawaida ni Tsh 21,000/-
Post a Comment