Rais wa Klabu ya Yanga atoa kauli hii kuelekea mechi za Klabu bingwa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Wakiwa wanajiandaa na mchezo wa raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Merrikh, Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Yanga, Injinia Hersi Said amesema wanaitaka rekodi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika


Septemba 16, mwaka huu Yanga itashuka ugenini kuvaana na Al Merreikh ya Sudan katika mchezo wa mkondo wa kwanza katika uwanja wa Pele mjini Kigali, Rwanda, kabla ya kurudiana jijini Dar es salaam kwenye Uwanja wa Azam Complex mwishoni mwa mwezi huu


Kuelekea mchezo huo kikosi cha Yanga kinajivunia kasi yao ambapo wamefuzu hatua ya kwanza ya awali kwa ushindi mnono wa mabao 7-1 wakiwatoa ASAS kutokea nchini Djibouti, huku pia wakiwa na mwenendo bora kwenye Ligi Kuu Bara anbapo wanaongoza msimamo na pointi zao sita walizokusanya kwenye michezo miwili ya kwanza


Msimu uliopita kikosi cha Yanga kwenye mashindano ya Kimataifa walianzia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo walitolewa hatua ya mtoano na kuangukia Kombe la Shirikisho Afrika ambapo walifanikiwa kumaliza washindi wa pili wa mashindano hayo


Akizungumzia ushiriki wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, Hersi amesema wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri 


"Kikosi kinaendelea na maandalizi ya mwisho ya michezo hii ya hatua ya mtoano, msimu uliopita tuliondolewa katika hatua kama hii na timu kutoka Sudan hivyo tunafahamu michezo hii"


"Lakini kama uongozi malengo yetu ni kuhakikisha tunaandika rekodi mpya katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama ambavyo tuliandika katika mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza fainali msimu uliopita"


"Tumeweka malengo ya kuingia hatua ya makundi, tunafahamu tuna zaidi ya miaka 20 hatujacheza hatua hii. Tukifanikiwa hatua hii tutakuwa na mkakati mwingine wa kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi katika hatua itakayofuata," alisema Hersi

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post