Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Hapa Tanzania kuna malalamiko kadhaa kuhusu waaamuzi kupendelea baadhi ya timu hasa wenyeji. Lakini haijafikia hii ninayotaka kukusimulia.
Haja ya ushindi inaonekana kuwa kubwa zaidi kwa baadhi ya timu kiasi kwamba mamlaka za klabu huamua kuwaadhibu waamuzi.
Nchini Uturuki, moja ya mataifa ambayo klabu zake zinaibukia na hata kusajili majina makubwa ya wanasoka kulitokea kioja miaka ya nyuma.
Mwamuzi Cagatay Sahan na wasaidizi wake walijikuta wakifungiwa ndani ya uwanja wa Trabzonspor kwa maagizo ya Rais wa klabu hiyo, yaani kama hapa kwetu zile timu pendwa za Kariakoo, basi viongozi wake wa juu watoe uamuzi huo.
Rais huyo, Ibrahim Haciosmanoglu alitoa uamuzi huo baada ya kufedheheshwa na mwamuzi huyo kusababisha timu kwenda sare ya 2-2 na Gaziantepspor.
Wenyeji waliona kwamba mwamuzi na wasaidizi wake waliwanyonga, kwani walitakiwa kuwapa penalti dakika za mwisho ambapo wangeishia kushinda 3-2 lakini wakapuuzia.
Kuona hivyo, baada ya mechi kumalizika, wakawakamata waamuzi na kuwafungia kwenye vyumba vya kubadilisha nguo na kuwaacha humo kwa saa kadhaa hadi wakawa wakanaribia kukata tamaa.
Haciosmanoglu anadai kwamba alitoa ruhusa kuachiwa kwa mwamuzi na wasaidizi wake baada ya Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kumpigia simu akimtafadhalisha kuwaachia maofisa hao.
Shirikisho la Soka la Uturuki likaanzisha uchunguzi juu ya suala hilo. Washabiki waliokuwa na hasira walikusanyika katika magenge nje ya uwanja huo wakimsubiri kwa hamu Sahan, lakni ilibidi waondoke baada ya kuona hatoki. Tukio hili ni la Oktoba 28 mwaka 2015.
Post a Comment