Morrison apewa masharti magumu FAR RABAT

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Winga wa zamani wa Yanga Bernard Morrison ‘BM’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa wa Morocco, FAR Rabat, huku akitakiwa kukaa ndani ya jengo la klabu lililopo katika kambi ya jeshi


Morrison ambaye ni raia wa Ghana, katika miezi hiyo 12 hatakiwi kufanya matukio yoyote ya utovu wa nidhamu na ikijitokeza mkataba wake utasitishwa mara moja na kuondoshwa klabuni.


Licha ya mkataba huo mgumu, lakini Morrison katika mazoezi ya wiki mbili aliyoyafanya na FAR Rabat amewashtua kwa kiwango kikubwa, huku baadhi ya mastaa wa timu hiyo wakishinikiza asajiliwe


Kocha Mkuu wa FAR Rabat Nasreddine Nabi ndiye aliyependekeza usajili wa Morrison baada ya kufanya nae kazi muda mfupi akiwa na Yanga


Hata hivyo Nabi aliwaambia mabosi wake wamfanyie Morrison majaribio na wakiridhika nae wamsajili lakini wahakikishe wanamuweka masharti magumu katika mkataba wake ili kulinda maslahi ya pande zote


Morrison anafahamika kwa vituko vyake alivyokuwa akifanya wakati anazitumikia klabu za Simba na Yanga za nchini Tanzania

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post