Mechi 170 za Championsih kuoneshwa mubashara

 Mechi 170 za Championsih kuoneshwa mubashara

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na televisheni za TV3 wameingia mkataba wa miaka 3 wa haki ya televisheni kuonesha ligi ya NBC championship (NBCCL).


Baada ya kutia kandarasi na wababe wa natangazo Star Times ili kurusha Mubashara mechi zaidi ya 170 za NBC Championship League ambayo inaendelea kuvuna udhamini mnono.


Huku ni msingi wa soka letu naamini kuna hatua kubwa sana itapigwa misimu kadhaa ijayo tutakuwa na ligi yenye ushindani mkubwa kuanzia NBC Championship League & NBC Premier League.


Msimamizi wa Vipindi wa Televisheni ya TV3, Emmanuel Sikawa akizungumza wakati wa Hafla ya kusaini mkataba wa haki za Televisheni kuonesha ligi ya NBC Championship wenye thamani ya shilingi milioni 613.


Aidha Sikiwa ameongezea na kusema “Mkataba huu utaanza mapema tuu baada ya hapa kumaliza kusaini hii leo na tunakwenda kuonesha zaidi ya mechi 170 Kwa sababu mbali mbali ambazo zimekwa wazi”


Kwa upande wa shirikisho la mpira Rais Wallace Karia alisema


“Kwanza nichukue nafasi ya kuishukuru serikali Kwa kuweka mazingira kwa wawekezaji wa Tanzania kuwekeza bila kubughudhiwa hivyo tumeingia mkataba mnono na Tv3 malengo ni kuweza kuikuza ligi yetu Kuwa bora”


Aidha Wallace Karia aliwakaribisha wageni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA) na Bodi ya Ligi Rwanda (RPLB) waliokuja kwa mafunzo ya kubadilishana uzoefu, wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa haki za televisheni kuonesha ligi ya NBC Championship.


"Leo TV3 tunaingia mkataba na TFF pamoja na Bodi ya Ligi kwa ajili ya kuonesha mechi za NBC Championship League kwa msimu huu 2023|24.


"NBC Championship 2023|24 itakuwa na mechi 240 sisi TV3 tutaonesha mechi zaidi ya 170, hatutaonesha mechi zote [240] kutokana na sababu kadhaa.


"Mechi hizo zitaonekana kupitia TV3 na TV3 Sports ambayo tutaizindua hivi karibuni na zinapatikana katika kisimbuzi cha StarTimes," amesema Emanuel Skawa, Msimamizi wa vipindi TV3.


"TV3 pamoja na TV3 Sports hivi karibuni zote zitakuwa kwenye mwonekano ang’avu yaani HD na sisi StarTimes tutashirikiana na TV3 kurusha vipindi vya maoni ya wadau wa soka kwenye mikoa mbalimbali inapochezwa NBC Championship League ili kukuza soka letu.


"StarTimes inaonekana zaidi ya nchi saba [7] Afrika [Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Zambia Mozambique na Afrika Kusini] huko mbele tunatarajia kufikia zaidi ya nchi 15 Afrika.


"Kutokana na kuonekana kwa StarTimes kwenye zaidi ya nchi saba za Afrika ni fursa kwa wachezaji wa NBC Championship League kuonekana na kupata nafasi ya kuuzika nje ya nchi.


"Sio lazima uwe na kisimbusi cha StarTimes lakini ukiwa na app [StarTimes On] utaweza kushuhudia mbashara mechi za Championship," amesema David Malisa, Mkuu wa Masoko StarTimes.


"Tukio hili ni la kihistoria kwa sababu kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka 11 tunaingia mkataba na TV ya nyumbani [TV3] kuonesha NBC Championship League.


"Ligi Kuu ya NBC ni namba tano [5] kwa ubora barani Afrika, Championship itapata nafasi ya kuonekana duniani na kuonesha ni jinsi gani ligi hii ni ngumu pengine kuliko hata NBC Premier League.


"Kuoneshwa kwa Ligi ya Championship kutaondoa malalamiko ambayo hayana msingi, watu walikuwa wanalalamika wanaonewa hata sehemu ambapo hawakuonewa," amesema Wallace Karia, Rais TFF.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post