Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Hukumu hiyo ilitolewa wiki iliyopita Agosti 31, 2023 na Jaji Irvin Mugeta wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam
Awali Bocco aliiomba mahakama iiamuru kampuni hiyo kumlipa Sh1 bilioni kama fidia, kutamka kuwa ilitumia picha yake bila kuwa na mamlaka nayo na kumlipa mrabaha wa asilimia 25 kipindi chote ilichoitumia
Tangazo hilo likiwa na picha ya Boko lililotolewa katika ukurasa wa Instagram wa kampuni hiyo kati ya Novemba 18, 2021 hadi Desemba 1, 2021 na ujumbe huo ulisomeka katika mtandao huo wa kijamii ukisema;
"Uhondo wa Ligi NBC unaendelea leo kwa mechi 3. Kubwa zaidi ni Simba watakuwa wageni wa Ruvu Shooting huko Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba. Siku za Pesa zimerejea,” na kusambaa ndani na nje ya Tanzania.
Bocco katika kesi hiyo aliyowakilishwa na mawakili Innocent Michael na Gadi Kabele, alisema kutumiwa kwa picha yake kulimaanisha amevunja mkataba wake na Simba na timu hiyo ilikuwa iko mbioni kumchukulia hatua za kinidhamu
Kesi hiyo namba 118 ya mwaka 2022 ilisikilizwa upande mmoja (ex parte) kwa kuwa mdaiwa aliondolewa katika mwenendo wa shauri hilo baada ya kushindwa kuwasilisha utetezi wake kwa maandishi kwa muda ulio ndani ya sheria
Kesi hiyo ilisikilizwa na Jaji Mugeta Agosti 25, 2023 na hukumu ikatolewa Agosti 31 na nakala ya hukumu hiyo kuwekwa katika mtandao wa mahakama (Tanzill) mahsusi kwa ajili ya kuchapisha maamuzi, sheria na kanuni bure mtandaoni
Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment