Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Lakred alitua nchini Ijumaa iliyopita na siku ya Jumamosi alikuwa sehemu ya wachezaji waliopata nafasi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kipanga Fc
Wanasimba huenda wakaanza kumuona langoni katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Power Dynamos
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 16 uwanja wa Levy Mwanawasa huko Zambia
Wakati Lakred akitua, mlinda lango namba moja Aishi Manula tayari ameanza mazoezi mepesi na pengine atakuwa tayari kurejea uwanjani katikati ya mwezi Oktoba
Manula anaweza kuwahi mchezo wa robo fainali Super Ligi dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Oktoba 20 na mchezo marudiano kupigwa Oktoba 24 huko Misri
Post a Comment