Kipa Mpya Simba kuanza majukumu kesho

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Mlinda lango Ayoub Lakred huenda kesho akaanza majukumu yake katika kikosi cha Simba kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Levy Mwanawasa huko Zambia

Tangu aliposajiliwa na Simba kutoka klabu ya FAR Rabat ya Morocco, Lakred bado hajatumika katika mechi ya mashindano

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira alimpa muda wa kuzoea mazingira pamoja na kuzoeana na wachezaji wenzake

Ni golikipa mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya Kimataifa kulinganisha na Ali Salim hivyo ni wazi Wanasimba watarajie kumuona uwanjani hapo kesho

Kipa huyo aliyesajiliwa kuziba pengo la Aishi Manula aliyeumia mwishoni mwa msimu uliopita na kufanyiwa upasuaji wa nyonga, alikosa mechi mbili za kimashindano ilizocheza Simba, ambazo ni zile za Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji, Simba ikishinda zote.

Hata hivyo, wakati wa mechi hizo alikuwa kikosini akijifua na kupata uzoefu na kujenga maelewano bora na wachezaji wenzake na kwa mujibu wa kocha wa makipa, Dani Cadena, Lakred yuko tayari kwa mchezo na watu watarajie kumuona kikosini Zambia.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post