Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchambuzi wa masuala ya michezo nchini, Oscar Oscar amesema kuwa wachezaji wa Klabu ya Simba wanaoongoza kwa kucheza rafu ni kiungo Sadio Kanoute na beki Henock Inonga Baka.
Oscar amesema hayo kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu kusema kuwa baadhi ya wachezaji wanatumwa kuwachezea vibaya wachezaji wa timu hiyo.
Haya yalijiri mara baada ya mchezaji wa Coastal Union, Haji Ugando kumchezea rafu Inonga na kusababisha kuondolewa uwanjani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
“Mchezo wa soka ni mchezo wa kiungwana sana alichokizungumza Mangungu baada ya mchezo ule ukimuuliza sasa hivi anaweza kusema tu kwamba ilikuwa rafu mbaya na akaondoa neno kuwa ilikuwa makusudi. Kwenye soka tumeshuhudia watu wakivunjwa miguu na wengine kupoteza maisha na madhara mengine makubwa sana.
“Hii ni physical contact game. Sio kwa nia mbaya lakini Henock Inonga huyu ambaye amekutwa na tukio hili na kumfanya asiendelee na mchezo, yeye pia ni bingwa wa rafu na ana matukio mengi amepandisha miguu juu kabisa dhidi ya wenzake.
“Lakini inatokea kwenye mchezo wa soka huwezi kusema imefanywa kwa makusudi na kijana yule wa Coastal kwa uungwana kabisa aliomba radhi baada ya mchezo.
“Wachezaji wa Simba hasa Henock Inonga wanakuwaga na michezo ya kihuni kupita maelezo, zile rafu za kihuni ambazo huwa anacheza, anakuwaga ametumwa na nani?
“Kwenye kikosi hiki cha Simba cha sasa, wana wacheza rafu mashuhuri wawili, wa kwanza ni Sadio Kanoute, anapiga buti huyu mtu. Nadhani ndiyo kitu anachokiweza zaidi uwanjani kuliko kitu chochote. Wao mpaka wamempa jina la Putin sijui ana‘put-in’ nini au Putin Rais wa Urusi? Wa pili ni Henock Inonga.
“Kama hatutaki kukubali na kuuheshimu mpira kwa sababu ni mchezo wa ‘physical contact’ watu wataumia tu, ila kama tutasema kila anayechezewa rafu basi kuna mtu upande wa pili kamtuma, niko pale ninasubiri mtu aniambie anayemtuma Putin ni nani, na anayemtuma Inonga ni nani?” amesema Oscar Oscar.
Post a Comment