Huyu hapa mwamuzi wa mechi ya Yanga vs El Merrikh September 30

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wiki ijayo Septemba 30 2023 Yanga itakuwa ikipigania nafasi adimu ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika katika mchezo wa marudiano dhidi ya Al Merrikh ya Sudan


Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kushinda au hata kupata matokeo ya sare ili kumaliza ukame wa kutocheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa zaidi ya miaka 24


Mwamuzi aliyepewa jukumu la kusimamia mchezo huo ni Tanguy Mebiani kutoka nchini Gabon


Yanga ikiwa mbele kwa ushindi wa mabao 2-0 waliopata nchini Rwanda wako katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi


Licha ya nafasi yao, kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanajiandaa kikamilifu na hawafikirii matokeo ya mchezo wa kwanza


Gamondi amesema bado kikosi chake hakijafuzu na amewataka wachezaji wake wasibweteke kwani kama wao waliweza kufunga mabao mawili ugenini hata wapinzani wao wanaweza kufanya hivyo jijini Dar es salaam


Al Merrikh wameanza 'mind games' mapema ambapo juzi zilisambaa taarifa kutoka Rwanda kuwa timu hiyo imewaondoa wachezaji 11 kikosini wakidaiwa kutokuwa sawa kisaikolojia wakiathiriwa na vita inayoendelea nchini kwao Sudan


Hata hivyo hizi zinaweza kuwa mbinu tu ili kuwafanya Yanga waamini mchezo wa pili utakuwa rahisi kwao

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post