Haji Manara kuachana na masuala ya soka

 Haji Manara kuachana na masuala ya soka

Baada ya kuwa nje ya Uwanja akitumikia adhabu yake ya kutojihusisha na soka kwa miaka miwili.


Aliyekuwa Afisa Habari wa YangaHaji Manara hii leo Septemba 17 akiwa nchini Uholanzi ametoa kauli ambayo imeshtua wengi akisema kuwa anafikiria kuachana na masuala ya Soka.


Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Manara ameandika;


“ Kwa sasa nafikiria kuachana na mambo ya mpira kabisa kwakuwa hata niliowategemea wanisemee na kukemea uonevu huo dhidi yangu uliopelekea kufungiwa kujishughulisha na masuala ya soka nao wamekaa kimya, ”


“ Hakuna haja ya kuendelea kuutumikia mchezo huu ninaoupenda kwakuwa wenye mamlaka ya mpira hawanjtaki na ni bora niende nikalime shungubweni, ”


“ kila nikiuliza nimekosa nini najibiwa nimemtukana Rais lakini kila nikiuliza ushahidi sipati majibu, iwapo Serikali au Chama changu kitaingilia jambo hili Tanzania itafungiwa na FIFA.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post