Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Aliyekuwa kiungo wa Yanga, Mrundi Gael Bigirimana amesajiliwa na timu ya Dungonnon Swifts inayoshiriki Ligi Kuu ya Ireland Kasikazini (NIFL Premiership).
Gael aliyewahi kuichezea Newcastle United ya Ligi Kuu England, alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu uliopita na kutambulishwa jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi uliukuwa ukifanyika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo Julai 9, 2022.
Hata hivyo staa huyo wa zamani wa Convetry City ya England alishindwa kuonyesha kiwango bora ndani ya Yanga iliyokuwa ikinolewa na kocha Nassredine Nabi kwa wakati huo.
Hali hiyo iliufanya uongozi wa Yanga, kumuondoa Gael kwenye usajili wa Ligi Kuu katika dirisha dogo la Januari mwaka huu ili kupata nafasi ya mchezaji mwingine wa kigeni ambapo ilimsajili beki Mamadou Doumbia kutoka Mali ambaye naye hakupata muda wa kutosha kucheza kikosini hapo.
Inafahamika kuwa baada ya Gael kuondolewa kwenye usajili wa Yanga ilihali akiwa bado ana mkataba na Wanajangwani hao, pande zote mbili zilikaa kujadili namna ya kuvunja mkataba huo na kukubaliana.
Hata hivyo Yanga haikukamilisha matakwa ya makubaliano ya pande zote mbili kwani haikumlipa pesa yake yote ya usajili (sign on fee), na Gael kuamua kuishitaki klabu hiyo kwenye Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) akifungua kesi ya madai.
Gael alishinda kesi hiyo, na FIFA kuiamuru Yanga imlipe kiungo huyo ndani ya siku 45 tangu ilipopewa taarifa lakini klabu hiyo haikufanya hivyo na Agosti 29, mwaka huu Yanga ilifungiwa na FIFA sambamba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufanya usajili hadi pale itakapomlipa mchezaji huyo.
Klabu ya Yanga ni klabu pekee ya Africa ambayo Bigirimana ameitumikia, kabla ya hapo hakuwahi kucheza soka Africa ngazi ya klabu.
Klabu alizopita mpaka sasa ni;
◉ Newcastle Utd — England
◉ Coventry city — England
◉ Rangers — Scotland
◉ Motherwell — Scotland
◉ Hibernian — Scotland
◉ Solihul Moors — Scotland
◉ Glentoran — Scotland
◉ Young Africans — Tanzania
◉ Dungannon Swift — Ireland Kaskazini
Gael Bigirimana alizaliwa nchini Burundi mwaka (1993), Mwaka (2004) aliondoka Burundi na wazazi wake akaelekea nchini England 'Ukimbizini' baada ya machafuko katika nchi yao ya Burundi.
Mwaka 2013, Gael akiwa na miaka (19) aliitwa kwenye timu ya taifa ya England Under 20. Hawa ni baadhi ya nyota walioitwa pamoja naye kwenye kikosi hicho;
◉ George Long
◉ John Stones
◉ Eric Dier
◉ John Flanagan
◉ Gael Bigirimana
◉ James Ward-Prowse
◉ Harry Kane
◉ Chris Long.
Post a Comment