Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Droo ya African Football League (Super League) inatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Septemba 02 huko Misri
Simba ni miongoni mwa timu nane ambazo zitashiriki michuano hiyo maalum ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika
Timu zimewekwa katika makundi mawili ya timu nne kulingana na alama walizokusanya katika mashindano ya CAF miaka mitano iliyopita
Kundi A lina timu za Al Ahly, Mamelod Sundowns, Wydad Athletic na Esperace
Kundi B lina timu za Simba, TP Mazembe, Enyimba na Perto Luanda
Timu za kundi moja hazitakutana kwenye hatua ya awali kwa maana timu kutoka kundi A zitapangwa kuchuana na timu kutoka kundi B
Simba itafungua michuano hiyo Oktoba 20 kwa kuchuana na Al Ahly, Mamelod Sundowns, Wydad au Esperance
Post a Comment