Alichokisema Ahmamed Ally baada ya Simba kupangwa na Al Ahly


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Baada ya Simba kumfahamu mpinzani wake katika michuano ya African Football League, mkakati wa kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika michuano hiyo umeanza mara moja


Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Wanasimba walisubiri kwa hamu droo hiyo iliyofanyika jana na kila mmoja amefurahi baada ya kupangwa kuikabili Al Ahly, mabingwa wa Afrika


Ahmed amesema furaha ya Wanasimba inatokana na historia yao ya kuwanyanyasa Al Ahly nyakati zote walipokuja Tanzania kucheza dhidi ya Simba


"Tulisubiri kwa hamu droo hii na sasa tumemfahamu mpinzani wetu ni Al Ahly, tumefurahi sana. Tunawakaribisha Dar, sisi tunataka kusimika ububwa wetu katika soka la Afrika, sasa ili uwe mkubwa lazima uwafunge wakubwa wenzio"


"Uzuri hata wao wanafahamu uchungu wa kucheza na Simba uwanja wa Benjamin Mkapa, wamepasuka mara mbili kwa mabao ya Meddie Kagere na Jose Luis Miquissone kilichobadlika ni kuondoka kwa Kagere lakini makali ya Simba yako palepale"


"Tunafahamu, ukitaka kuwa mkubwa jela lazima umpige bwana jela, kwa hiyo tunamkaribisha Al Ahly na tunamuhakikishia kwamba tutahangaika nae"


"Super Ligi hairuhusiwi kwa watoto wadogo, hii ni kwa ajili ya wakubwa pekee na Simba Sc ni mkubwa, kwa hiyo hatuna mashaka, hatuna hofu, hatuna wasiwasi wala hatuna woga, " alitamba Ahmed

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post