Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya mtangazaji Jemedari Said kuwakosoa Yanga juu ya ishu ya kusema mabasi yanayosafiri na mashabiki kwenda Rwanda yatakuwa na viongozi wa Yanga halafu isiwe kweli, Meneja wa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally ameibuka na kukazia suala hilo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed Ally amekazia maneno ya Jemedari bila kutaja jina la klabu husika lakini inaonesha kabisa analenga Yanga.
"Niliwaambia hawa watu ni Fix yaani waongo waongo. Imagine walikua na ujasiri wa kusema mchezaji kaitwa timu ya Taifa ya Uganda hawashindwi kutoa idadi ya uongo ya mabasi.
"Hii yote ni shida ya kutaka kushindana na wenye shughuli zao. Na hii ni shida ya kuiga kila kitu.
"Wanapenda Fix Fix ndo maana wanashadadia eti wao ni watatu kwa ubora Afrika, Yaani timu ina miaka 50 haijacheza Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika halafu iwe nafasi ya tatu kwamba mmmetuaonaje Waafrika.
"Nawepeni tahadhari msiseme uongo kwenye Nchi ambayo Jemedari Said yupo atawaumbua tuuu," aliandika Ahmed.
Post a Comment