Ahmed Ally apewa za uso kisa beki wa Yanga

 Ahmed Ally anaidharaulisha Simba Sc - Mchambuzi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mchambuzi wa mbio za magari Albogast Myaluko kupitia Kipenga ya East Africa Radio, amemjia juu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally aliyesema beki wa Yanga, Gift Fred hana kiwango cha kuitwa timu ya taifa.


Fred aliitwa Timu yake ya Taifa ya Uganda kwa ajili ya michuano ya kufuzu Fainali za AFCON 2023, lakini baadaye alipata majeraha kisha kuachwa na Kocha Micho ambapo alirejea kwenye Klabu yake ya Yanga.


"Kuna namna hawa maafisa Habari wanajikuta wanadharaulisha timu zao na wachezaji wao wenyewe wakiamini wanawadharaulisha watani wao.


"Unaposema beki wa klabu ya Yanga hana kiwango cha kuitwa National Team wakati Che Malone yupo kambini Bunju, hapo umelinda brand yako au umeeleza kwamba mchezaji ambaye hajaitwa hana kiwango.


"Huoni kwamba hii inakurudia wewe mwenyewe, maana yake hapa hujalinda brand yako, ni kama unataka kulinganisha sasa kwamba sisi wote tuna wachezaji wabovu ambao hawajaitwa timu za taifa. Unamsema Gift Fred mbona Che Malone hajaitwa timu ya taifa?," amesema Albogast.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post