Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amekosoa suala la Yanga SC kuwapa mbinu Singida FG kuelekea mchezo wao wa Kimataifa.
Ahmed amesema, badala ya Yanga kuwapa mbinu, wao ndio wanapaswa kuwapa mbinu wote wawili sababu wote ni wageni kwenye mashindano hayo makubwa.
"Wote ni wageni, sisi ndio tunawaambia watu vipi wacheze na nini wanatakiwa kufanya. Tutawaambia kwenye vikao vya umoja wa klabu, tutawaambia sisi si wachoyo na suala la kufanikiwa litabakia kwa wenyewe.
"Lazima tuwaambie kama klabu role model wa vilabu vingi Afrika Mashariki. Sisi ndio tuna mafanikio makubwa zaidi kwenye mashindano haya hivyo lazima tuwape mbinu wote wanaokuja," alisema Ahmed.
Post a Comment