Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya kukamilika raundi mbili za mwanzo, Yanga imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama sita sawa na Azam Fc na Simba lakini Wananchi wana utajiri mkubwa wa mabao ya kufunga
Wakati Azam Fc wakifunga mabao saba na kuruhusu bao 1, Simba wamefunga mabao sita na kuruhusu mabao mawili huku Wananchi wakifunga mabao 10 pasipo kuruhusu bao lolote
Kamwe amesema wamepania kuweka rekodi ya aina yake baada ya mechi 10
"Hii kasi tuliyoanza nayo haitapoa, tunataka baada ya mechi 10 tuwe na mabao 50 na alama 30,"alitamba Kamwe
Yanga ilianza kutetea ubingwa wake kwa kuibamiza KMC mabao 5-0, kisha JKT Tanzania wakafuatia kukumbana na kipigo cha mabao 5-0 pia
Katika mechi nane zitakazofuatia, mchezo dhidi ya Simba ni miongoni ukitarajiwa kupigwa Novemba 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Wakati mchezo dhidi ya Namungo Fc ukiwa bado haujapangiwa tarehe, mchezo utakaofauata kwa Yanga ni dhidi ya Ihefu Fc, utapigwa Oktoba 04 uwanja wa Highland Estates mkoani Mbeya
Huu utakuwa mchezo wa kisasi kwa Yanga kwani Ihefu Fc ilichafua rekodi ya Wananchi kutopoteza mechi kwenye ligi msimu uliopita
Wananchi walikuwa wamecheza mechi 49 pasipo kupoteza lakini wakapoteza mechi ya 50 kwa kufungwa mabao 2-1 na Ihefu Fc
Post a Comment