Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Yanga imemtambulisha Alaa Meskini kuwa mkufunzi wa magolikipa akichukua nafasi ya Milton Nienov aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake kumalizika
Meskini tayari alishaanza majukumu yake katika benchi la ufundi chini ya Kocha Miguel Gamondi ambaye ndiye aliyependekeza aongezwe
Meskini amewahi kuzinoa klabu za Wydad Athletic (Morocco), Hassania D'agadir (Algeria) na timu ya vijana U23 ya FAR Rabat ya Morocco
Benchi la ufundi Yanga sasa linaundwa na makocha ambao wote wamewahi kufanya kazi katika nchi za Afrika Kaskazini kama Morocco, Tunisia, Misri na Algeria
Mataifa haya yametawala soka la Afrika ngazi klabu na hata timu za Taifa, Yanga ina malengo makubwa katika soka la Afrika
Post a Comment