Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Asubuhi Yanga ilicheza na Friends Rangers na jioni ikashuka tena dimbani kuikabili JKU
Kilikuwa kipimo cha mwisho kwa kikosi kabla ya kuelekea mkoani Tanga kushiriki Ngao ya Jamii
Katika wiki tatu za pre-season, Yanga imecheza michezo minne ya kirafiki ikishinda mitatu na kutoka sare mchezo mmoja
Walianza kwa kuichapa Kaizer Chiefs bao 1-0, wakaichapa Magereza Dar mabao 10-0 jana asubuhi wakaichapa Friends Rangers mabao 6-1 na jioni kutoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya JKU
Katika mechi hizo Yanga imefunga mabao 17 huku ukuta wake ukiruhusu bao moja. Wapo ambao watasema baadhi ya mechi zilikuwa nyepesi lakini ni aina ya mechi ambazo zimemsaidia Gamondi kubaini ni kiasi gani wachezaji wake wanaweza kutengeneza nafasi na kuzitumia
Kimbinu, Gamondi hatofautiani sana na kocha aliyepita Nasreddine Nabi, kilichoongezeka kwa Gamondi ni kuwa timu yake inacheza kwa kasi zaidi
Gamondi haruhusu mchezaji kukaa na mpira muda mrefu, ukipigiwa pasi unaachia kisha unawahi kwenye nafasi
Yanga inajenga mashambulizi kutokea nyuma lakini wakivuka katikati ya uwanja kasi inaongezeka
Wakati mwingine timu inaposhambulia walinzi wa pembeni wanaingia kati eneo la kiungo huku mawinga wakikimbiza pembeni na kupiga krosi
Mashabiki wa Yanga watarajie kushuhudia soka lenye kasi ya aina yake, hakuna shaka msimu huu Yanga itafunga mabao mengi Kumbuka mechi zote za ligi kuu zitaoneshwa live kwenye app yetu Bure hivyo kama bado hujaipakua bofya hapa
Post a Comment