Yanga watoa kauli hii kuhusu sakata la Bigirimana - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga watoa kauli hii kuhusu sakata la Bigirimana

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Yanga itamlipa kwa awamu aliyekuwa kiungo wake Gael Bigirimana


Kulikuwa na mvutano kati ya uongozi wa Yanga na mchezaji huyo juu ya malipo aliyokuwa akihitaji ili kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliokuwa umebaki hivyo kupelekea pande hizo kupelekana FIFA kwa ajili ya kupata suluhisho


FIFA ikatoa maamuzi  ya kuitaka Yanga imlipe Bigirimana kiasi cha fedha walichokuwa wamekubaliana na kwa kuwa Yanga ilichelewa kukamilisha malipo ya awamu ya kwanza ambayo walipaswa kulipa ndani ya siku 45 tangu hukumu ilipotolewa, juzi TFF wakatoa taarifa kuwa Yanga imefungiwa na FIFA kusajili hadi hapo watakapomlipa mchezaji huyo


Kamwe amethibitisha kuwa mchakato wa malipo ya Bigirimana unaendelea huku akiwatoa hofu Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuwa jambo hilo litamalizwa hivi karibuni


Dirisha la usajili linafungwa leo, ahueni kwa Yanga ni kuwa hukumu hiyo imetolewa wakati wakiwa tayari wamekamilisha michakato ya usajili katika dirisha hili  


Ili Yanga iweze kusajili wachezaji katika madirisha yajayo ni lazima ikamilishe malipo ya Bigirimana ambaye usajili wake ni kama umesababisha hasara tu kwani hakufikia hata nusu ya kile ambacho wengi walitarajia kutoka kwake hasa ikizingatiwa ni mchezaji aliyewahi kucheza ligi kuu ya Uingereza



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz