Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Beki wa kati wa Simba Hennock Inonga leo atafanyiwa vipimo kubaini ukubwa wa jeraha alilopata
Hennock alishindwa kumaliza mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Singida FG jana baada ya kuumia bega
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Inonga atafanyiwa uchunguzi wa kitabibu leo, Wanasimba watapewa taarifa kuhusu hali yake
"Ni kweli Inonga aliumia jana, alitoka uwanjani akiwa na maumivu makali sana ya bega. Alipatiwa huduma ya kwanza, sasa anaendelea vizuri. Kesho (leo) Madaktari watamfanyia vipimo kubaini ukubwa wa jeraha ili kuona kama atahitaji matibabu zaidi au la," alisema Ahmed
Simba ilitinga fainali ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Singida FG
Siku ya Jumapili, Simba itachuana na Yanga katika mchezo huo wa fainali kumbuka mchezo huo utaoneshwa mubashara kwenye app yetu na kama bado hujaipakua BOFYA HAPA
Post a Comment