Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Association Sportive d'Ali Sabieh Djibouti Telecom (ASAS Fc) ni klabu kutoka Djibouti, wanashiriki kwenye ligi kuu ya Djibouti
Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1991, inamiliki uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Aptidon, wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000.
ASAS FC wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Djibout mara saba na Djibouti Cup mara tatu ndio klabu iliyofanikiwa zaidi nchini humo
Hawajawahi kuvuka hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa wala kombe la Shirikisho barani Afrika
Msimu uliopita ilishiriki kombe la Shirikisho ikatupwa nje hatua ya awali kwa kufungwa bao 1-0 na AS Kigali ya Rwanda
Jumapili ya wiki hii watakuwa Tanzania kuchuana na Yanga katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika
Kwa kuwa uwanja wao haukukidhi vigezo vya CAF, timu hiyo imelazimika kucheza mechi yake ya nyumbani katika uwanja wa Azam Complex
Mchezo wa kwanza ukipigwa August 20 wakiwa wenyewe na mchezo wa pili utapigwa August 28 Yanga wakiwa wenyeji
Mechi zote mbili kupigwa Tanzania ni faida kubwa kwa Yanga, vijana wa kocha Miguel Gamondi wana kazi ya kuhakikisha wanamaliza mechi Jumapili ili mchezo wa marudiano uwe wa kukamilisha ratiba tu
Post a Comment