Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Licha na Kumwembe na Jemedari Said, Pia Edgar Kibwana naye amefungukia hilo mara baada ya Simba kuibuka mshindi katika mchezo huo kwa penati 3-1 huku Yanga wakikosa penati 3.
Edo Kumwembe; "Ahhhh ndio maana kila siku napoteza mapenzi na huu mchezo. Mchezo umekuwa laini sana Well, nasikia hii habari ya kwamba KIpa wa Simba, Ally alikuwa ameondoka haraka katika mstari ndo maana Yanga wakakosa penalti.
Guys haya masheria yenu yameanza sasa hivi. Zamani wakati nacheza, kipa atoke kabla au asubiri lazima penalti yangu iende nyavuni.
Am sure wachezaji wa Yanga waliokosa penalti zao wanajilaumu wenyewe kwa upigaji wa kibwege kuliko Ally kuwahi kutoka katika mstari. Hatua 12 ni karibu mno mtu kutupia kunyavu," Edo Kumwembe.
Jemedari Said Bin Kazumari; "Nawapongeza Simba SC kwa kutwaa Ngao ya Jamii, nampongeza kijana wangu Ally Salim kwa kuzuia penati 3 ni ushujaa mkubwa.
"Zaidi nampongeza Ally Salim kwa mbinu yake ya kutoka hatua moja mbele kabla mpira haujapigwa na kumuibia mpigaji na mwamuzi msaidizi ambaye huwa ndo mwenye shughuli ya kuangalia kama kipa ametoka kabla ya mpira kupigwa.
"Ukiangalia penati zote Ally Salim alikuwa anatangulia kutoka kabla mpira haujapigwa hata ile moja aliyofungwa pia ni vile mpira ulikuwa na kasi.
"Nampongeza Ally Salim kwa mbinu hii ambayo leo imemsaidia kwa kutokuwa na waamuzi makini pia, lakini nampa tahadhari mbinu hii siku hizi ni HARAMU na ikitokea ukaokoa basi penati inarudiwa, hivyo leo penati zote 3 zingerudiwa, ukibisha angalia Video kwa umakini.
"Diarra anaweza kuwa mwalimu mzuri kwa namna alivyookoa penati yake kwa kuhakikisha mguu mmoja unabaki kwenye mstari wakati mpira unapigwa na sio kutokea mbele hatua moja.
"Simba furahieni leo na Ngao mmebeba ila kwenye mechi zenye waamuzi makini msije mkarusha ngumi tu, kipa anatokea mbele hatua moja kabla mpira kupigwa ambayo ni makosa," amesema Jemedari Said.
Edgar Kibwana, Clouds Media; "Ally Salim anastahili pongezi nyingi kwa kile alichokionyesha katika mchezo dhidi ya Yanga, kudaka penalty 3 dhidi ya wana fainali sio mchezo.
Lakini kuna jambo ambalo halikua sawa kwa upande wa waamuzi ambao ndio wenye jukumu la kusimamia sheria zote uwanjani.
Kikawaida Golikipa wakati wa kudaka penalty hapaswi kutoa miguu yake yote kabla mpigaji hajapiga mpira lakini kwa Ally Salim ilikuwa tofauti, alikua anatoka hata kabla mpira haujapigwa.
Katika penalty zote tatu alizocheza zilistahili kurudiwa kwani zilikuwa zinapigwa wakati ambao ameshatoka kwenye mstari. Bado tuna safari ndefu sana kuhusu waamuzi wetu na sheria hizi," amesema Edga Kibwana.
Post a Comment