Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba imerejea Tanzania Alfajiri ya leo wakitokea Uturuki ambako waliweka kambi ya wiki tatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya
Robertinho amewapongeza viongozi wa Simba kwa kufanya usajili makini ambao umeweka uwiano sawa katika kila nafasi
"Nawapongeza sana viongozi wa Simba kwa kusajili wachezaji wazuri. Sasa nina vikosi viliwi vyenye uwiano sawa. Kama mchezaji mmoja anakosekana kwa sababu ya majeraha au yoyote, naweza kuweka mwingine pasipo kuathiri ubora wetu"
"Hili ni jambo muhimu sana kwa timu yenye malengo ya kushindania mataji. Tunawaheshimu wapinzani wote tutakaokutana nao lakini ifahamike malengo yetu ni kushinda mataji," alisema Robertinho
Msako wa mataji utaanza wiki ijayo kwenye Ngao ya Jamii ambapo August 10 Simba itacheza na Singida FG mchezo wa nusu fainali ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani
Robertinho na vijana wake wataanza kutoa burudani kwenye SIMBA DAY Jumapili ambapo Simba itacheza na Power Dynamo uwanja wa Benjamin MkapaAmbapo mechi itakuwa LIVE bure kwenye App yetu unaweza kuidownload Sasa bofya hapa
Post a Comment