Tuko tayari kwa Ngao ya Jamii - Skudu

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kiungo mshambuliaji wa Yanga Skudu Makudubela amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wako tayari kwa mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumatano, August 09 katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga


"Wachezaji wote wako tayari, sote tuko imara, tunasubiri kwa hamu Ngao ya Jamii tuuwashe moto"


"Tumefanya maandalizi muhimu kuhakikisha tunakuwa timamu, hatutajali mpinzani tunayekutana nae, tumejiandaa kimbinu, kiakili na kimwili"


"Tunasubiri kwa hamu kuanza kwa mashindano hayo ya Ngao ya Jamii," alisema Skudu


Nae kiungo Zawadi Mauya amesema kikosi kimeimarika na wako tayari kukabiliana na Azam Fc katika mchezo ambao wanatarajia hautakuwa mwepesi


"Sisi tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Azam Fc August 09, tunafahamu mchezo hautakuwa mwepesi kwa sababu Azam Fc wameimarisha kikosi chao kama ilivyokwetu, kuna wachezaji wapya wamekuja kuchukua nafasi za wale walioondoka"


"Tumepokea maelekezo ya walimu mazoezini dhamira yetu ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo na kutinga fainali"

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post