TFF yawabana wachezaji mikataba binafsi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Jana Bodi ya Ligi ilitangaza marekebisho na maboresho ya kanuni toleo la 2023 ambapo hivi sasa ikiwa mchezo ataingia makubaliano na benki nyingine tofauti na NBC basi hataruhusiwa kutangaza


Katika marekebisho hayo, mchezaji atakayekiuka atakabiliwa na kufungiwa kwa kipindi cha kati ya mwezi mmoja na mitatu


Kwa mujibu wa kanuni namba 16: 1:12 katika maboresho: "Hairuhusiwi kwa mchezaji kuingia mkataba binafsi wa udhamini na mshindani wa kibiashara wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu, atakayekiuka atafungiwa kwa kipindi cha kati ya mwezi mmoja na mitatu"


Akitoa maoni yake, Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick ambaye ni mmoja wa Wanasheria wa FIFA, amesema kanuni yoyote kwenye mikataba ya kibiashara hutengenezwa kwa manufaa ya mpira, timu na wachezaji


"Kama waliopitisha hii kanuni wameona ina masilahi kwa wachezaji wetu na mpira kwa ujumla wake, basi sawa! Si vibaya tukaiga mambo mazuri kwa wenye soka lao, wenzetu sikuhizi hawatoi tena exclusive rights kwa wadhamini," aliandika Simon kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii


Ni wazi mabadiliko haya yanakwenda kuwaathiri Stephane Aziz Ki na Farid Mussa ambao waliingia mikataba na benki ya CRDB

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post