Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo wa kwanza wa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Asas Fc ya Djibout dhidi ya Yanga utapigwa Jumapili August 20 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wamepokea maelekezo kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuwa mechi zote za hatua ya awali dhidi ya Asas Fc zitapigwa uwanja wa Azam Complex
Mchezo wa kwanza utapigwa Jumapili ijayo na mchezo wa pili utapigwa Jumapili ya wiki itakayofuata, August 28 katika uwanja wa Azam Complex
Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo kuwa VIP A 30,000/-, VIP B 20,000/- na Mzunguuko 5,000/-
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kununua tiketi mapema kwa kufahamu idadi ya mashabiki ambao wanaruhusiwa kuingia uwanja wa Azam Complex
Post a Comment