Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mashabiki wa Simba wana shauku kubwa ya kumuona winga Aubin Kramo aliyetua Msimbazi kutoka klabu ya Asec Mimosas katika dirisha hili la usajili
Kramo alicheza kwa takribani dakika 15 kwenye mchezo wa Simba Day dhidi ya Power Dynamo, tangu wakati huo hajaonekana tena uwanjani
Daktari wa Simba Edwin Kagabo amesema winga huyo ni majeruhi, alipata majeraha kabla ya Ngao ya Jamii
"Kramo aliumia mazoezini wakati tukijiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida BS, tunashukuru hali yake inaendelea vizuri," alisema Kagabo
Kramo alikosa mechi zote mbili za Ngao ya Jamii dhidi ya Singida BS na Yanga na pia mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar
Wanasimba watarajie kumuona uwanjani karibuni
Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Post a Comment