Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally, amesema mkakati wa Simba ni kuibuka mabingwa wa Ngao ya Jamii
Simba ilitua Tanga jana majira ya usiku na leo inatarajiwa kukamilisha maandalizi kabla ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Fountain Gate. Mchezo huo utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Mkwakwani
"Tunashukuru tumefika salama mkoani Tanga. Leo tutakuwa na nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho majira ya saa 11 jioni"
"Sisi hatukuja hapa Tanga kutembelea, tumekuja kuchukua Ngao ya Jamii. Tumejiandaa vizuri na pia tuna kikosi bora, hivyo hakuna mjadala kuhusu hilo, kauli mbiu yetu ni kuwa TUMEKUJA TANGA KUCHUKUA NGAO YA JAMII," alisema Ahmed
Katika hatua nyingine, Ahmed amesema mshambuliaji Moses Phiri ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na timu mkoani Tanga
Ahmed amesema Phiri yuko fit kwa asilimia 100 na uongozi unamtekelezea mahitaji yake yote
"Phiri ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na timu mkoani Tanga, suala la kucheza au la linabaki mikononi mwa benchi la ufundi. Lakini sisi upande wa uongozi tumetimiza kile ambacho tunapaswa kufanya kwa mchezaji"
"Wanasimba wapuuze taarifa za upotoshaji kwani hakuna kiongozi anayeweza kumzuia Phiri asicheze. Haiwezekani klabu imlipe fedha nyingi halafu tumzuie asicheze, hilo haliingii akilini"
"Ni kweli Wanasimba wanataka kumuona Phiri uwanjani, hata sisi viongozi tunatamani kumuona Phiri uwanjani kwani ni mchezaji bora lakini bado mwenye maamuzi ya mwisho ni kocha Robertinho," alisema Ahmed kumbuka mechi hii itakuwa Live Bure kwenye app yetu kama bado hujaipakua Bofya HAPA
Post a Comment