Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wakati huu wa mapumziko ya kalenda ya CAF, kikosi cha Simba huenda kikaelekea nchini Kenya kuweka kambi ya muda mfupi kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi, utapigwa Septemba 16 kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa huko Zambia
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amehitaji kupata mechi tatu za Kimataifa za kirafiki kama sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha Simba inatinga makundi ya ligi ya mabingwa
Gor Mahia, Polisi Kenya na Bandari zinaweza kuwa miongoni mwa timu ambazo Simba itacheza nazo huko Kenya
Baada ya mapumziko ya siku chache, Simba ilirejea kambini Bunju juzi na jana kuanza mazoezi rasmi
Post a Comment