Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Jana kiungo wa Azam Fc James Akaminko aliwanyima Wananchi wa Tanga kushuhudia burudani kutoka kwa Waziri wa raha Skudu Makudubela ambaye aliumia kwenye dakika ya tano ya mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii akifanyiwa madhambi na Akaminko
Skudu alishindwa kuendelea na mchezo huo kulazimika kutolewa nje kwenye dakika ya saba nafasi yake ikichukuliwa na Chrispine Ngushi
Uongozi wa Yanga umebainisha kuwa Skudu anaendelea vizuri ambapo atafanyiwa vipimo zaidi leo
Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema Skudu alipewa dawa ya kutuliza maumivu ya goti, hali yake ikiwa ni nzuri sasa
Hata hivyo Etutu amesema watamfanyiwa vipimo zaidi baada ya saa 24 ili kubaini kama atahitaji matibabu zaidi au apewe mapumziko tu
Skudu huenda akarejea tena uwanjani kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba au Singida FG siku ya Jumapili
Post a Comment