Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Unaweza kusema kiungo Khalid Aucho ameanza na gia kubwa msimu huu. Kiungo huyo wa Kimataifa kutoka Uganda alin'gara katika kikosi cha Yanga kwenye mechi mbili za Ngao ya Jamii mkoani Tanga
Msimu uliopita alikuwa chaguo la kwanza kwa Kocha Nasreddine Nabi katika eneo la kiungo na mapema tu msimu huu amekuwa chaguo la kwanza kwa Miguel Gamondi
Pamoja na ubora wa wachezaji waliosajiliwa na Yanga katika eneo la kiungo, Aucho ameendelea kuwa na 'kiti cha kudumu' katika kikosi cha kwanza
Habari njema ni kuwa adhabu yake ya kufungiwa mechi mbili na CAF ilimalizika baada ya kukosa mechi zote za fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger msimu uliopita
Hakuna shaka Jumapili atakuwepo uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya ASAS Fc
Post a Comment