Skudu kamili kurejea kikosini

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kiungo mshambuliaji wa Yanga Skudu Makudubela leo anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi leo kabla ya kuungana na wenzake kwenye maandalizi ya mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Skudu yuko tayari kurejea uwanjani


"Baada ya timu kurejea Dar es salaam kutoka Tanga, leo tunaanza mazoezi Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc ambao utapigwa Jumapili ijayo"


"Mchezaji wetu Skudu, leo ataanza rasmi mazoezi mepesi baada ya vipimo vya kitatibu kubainisha kuwa amepona majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya Azam Fc"


"Tunatarajia atajumuika kwenye mazoezi na wenzake ndani ya muda mfupi na pengine Jumapili kutegemea na mpango wa mwalimu, anaweza kuwa sehemu ya wachezaji watakaoikabili Asas Fc," alisema Kamwe

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post