Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba imeachana na golikipa Jefferson Luis aliyebainika kuwa na majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu
Jefferson alikuwa kwenye kambi ya Simba Uturuki lakini uongozi ulichukua hatua ya kuachana nae baada ya vipimo kubaini ana majeraha makubwa
"Suala la golikipa tutatoa taarifa muda sio mrefu, kabla ya SIMBA DAY kila kitu kitakuwa kimewekwa hadharani," aliserma Ahmed
Simba imerejea nchini alfajiri ya leo Jumatano baada ya kumaliza kambi ya wiki tatu huko Uturuki
Ally Salim na Feruz aliyepandishwa kutoka timu ya vijana ndio magolikipa ambao kwa sasa wako kikosini
Hata hivyo habari njema kwa Wanasimba ni kuanza mazoezi mepesi kwa mlinda lango namba moja Aishi Manula ambaye anaweza kurejea uwanjani mapema
Usikose kutazama mubashara Simba Day Bure kabisa download app yetu Ili kutazama bofya hapa sasa
Post a Comment