Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ni baada ya Power Dynamos kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Stars jana na hivyo kufuzu raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini baada ya kuchapwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Mchezo wa kwanza utapigwa Septemba 15 huko Zambia na mchezo wa marudiano kupigwa Septemba 29 jijini Dar es salaam
Simba na Power Dynamos zilichuana kwenye Tamasha la Simba Day, Wekundu wa Msimbazi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Timu hizo zinakutana tena mara mbili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi
Wakati Simba ikichuana na Power Dynamos, Watani zao Yanga wao watachuana na El Merrikh ya Sudan
Jana Yanga ilitinga raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 dhidi ya Asas Fc ya Djibout wakati El Merrikh walifuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Otoho ya Congo Brazaville
Simba na Yanga zote zitaanzia ugenini katika mechi za kwanza na kumalizia nyumbani mechi zao za marudiano
Post a Comment