Simba kusafirisha mashabiki Zambia

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Simba imetoa fursa kwa mashabiki kusafiri na timu Zambia katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos ambao utapigwa Alhamisi, Septemba 16 huko Zambia


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kutakuwa na usafiri wa basi kwenda Zambia na kurudi


"Kuelekea mechi yetu dhidi ya Power Dynamos tunategemea kupeleka mashabiki kama ilivyo kawaida yetu tunapokuwa na mechi kwenye nchi za jirani tunatumia basi kupeleka mashabiki"


"Bahati nzuri Zambia tumeshawahi kwenda huko. Tulipokea maoni tutumie treni na tukafanya mazungumzo na wakawa tayari kutupa punguzo maalumu lakini ratiba za safari ya treni zinapishana na mechi yetu. Utaratibu ambao umeandaliwa na Simba ni tutatoa basi hadi Ndola, Zambia na litarejea nchini baada ya mechi"


"Basi litaondoka nchini kwenda Zambia tarehe 13, Septemba saa 1 usiku na tutafika Ndola, Zambia tarehe 15, Septemba. Tarehe 17, Septemba baada ya mechi basi litaanza safari kurudi Tanzania"


"Kwa yeyote ambaye anataka kuungana nasi afike ofisini. Kwa kila mtu gharama ni Tsh. 200,000 na anatakiwa kuwa na pasi ya kusafiria na kadi ya manjano. Mwisho wa kupokea nauli ni tarehe 10, Septemba," alisema Ahmed


Akizungumzia maandalizi ya ya kikosi, Ahmed amesema timu imeingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Power Dynamos


Kutokana na muda mrefu uliopo kuelekea mchezo husika, Simba huenda ikaweka kambi nchi jirani kwa ajili ya maandalizi


"Tuna siku nyingi za kufanya mazoezi na hivyo menejimenti inaangalia namna gani kikosi kitaweka kambi ya kujiandaa. Mazungumzo yamejikita katika sehemu mbili, moja kuweka kambi kwenye nchi za jirani au tuweke kambi ndani ya Tanzania katika maeneo mengine."


"Katika kipindi chote cha kambi tunatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki. Tunasubiri uthibitisho wa timu ambazo tutacheza nazo, moja ya nje na nyingine ya ndani. Lengo letu kama Simba ni tupate mechi ngumu, mechi ya kiushindani," alisema

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post