Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Afisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda amesema, ratiba rasmi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier Ligue) itatangazwa hivi karibuni.
Akizungumza na Wasafi FM leo Agosti 4, 2023, Boimanda alisema, anafahamu kuwa wanazi wa Ligi Kuu wanatamani kuiona lakini kulikuwa na sababu ambazo zimewafanya wachelewe kutangaza.
"Ratiba ya FIFA ilichelewa na kama unavyojua sisi lazima tusubiri kwanza ratiba ya FIFA ndio tuweze kupanga ya kwetu lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa, tupo kwenye hatua ya mwisho na muda sio mrefu itakuwa hadharani," alisema Boimanda.
Boimanda aliwahakikishia mashabiki wa soka kuwa, ratiba hiyo itatoka kabla ya mechi ya uzinduzi wa Ligi, mechi za Ngao ya Jamii zinazotarajia kuanza wiki ijayo.
Mechi zote za ligi kuu tutazionesha live bure kwenye app yetu bofya hapa kuidownload sasa
Post a Comment