Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Chama aliyewahi kuitumikia Power Dynamos kwa miezi sita kabla ya kusajiliwa na Simba msimu wa 2018/19, amesema Power Dynamos ni moja ya timu bora na zenye historia kubwa nchini Zambia
"Power Dynamos ni timu kubwa sana Zambia, wakati naanza kucheza mpira ligi kuu, msimu wa 2009/10, ndoto yangu kubwa ilikuwa kuichezea Power Dynamos, nashukuru nilicheza kwa muda mfupi kabla ya kusajiliwa na Simba"
"Ni timu nzuri walipotea kwa misimu kadhaa lakini nafurahi kuona wamerejea tena wakishinda ubingwa wa Zambia. Natarajia utakuwa mchezo mzuri kwa timu zote"
"Mimi nawaombea washinde mechi yao ya ligi ya mabingwa ili tukutane nao tena ili tuwapige..," alisema Chama
Simba na Power Dynamos zinaweza kukutana kwenye raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Afrika kama Dynamos watashinda mchezo wa hatua ya awali dhidi ya African Star ya Namibia kwani mshindi wa mchezo huo atakutana na Simba inayoanzia raundi ya kwanza
Post a Comment