Polisi wabaini tiketi bandia za Simba Day

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewataka watu wote wasiokuwa na tiketi za kuingilia kwenye tamasha la Simba Day wasijaribu kabisa kuusogolea uwanja wa Benjamin Mkapa leo, kwani wanaweza kuwa ndiyo chanzo cha msongamano.


Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Jumanne Muliro, jana na kusema kwamba watakaokiuka watachukuliwa hatua, na kwamba limebaini uwepo wa watu wanaouza tiketi bandia licha ya tiketi zote za tamasha hilo kuuzwa (Sold out).


"Jeshi la Polisi linazo taarifa kuwa kuna makundi ya watu wanazo tiketi za bandia na sasa wanaanza kuziuza kwa baadhi ya watu, Jeshi la polisi linawatahadharisha watu kuwa makini na kuuza ama kununua tiketi hizo, kwani linafuatilia sana kwa makini kundi la matapeli hao, hata hivyo ulinzi umeimarishwa siku moja kabla," amesema Kamanda Muliro

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post