Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo huo utapigwa Jumatano, August 09 katika uwanja wa Mkwakwani
Yanga inatarajiwa kuhitimisha pre-season kwa mchezo mmoja wa kirafiki ambao utapigwa Avic Town
Awali mabingwa hao wa Tanzania Bara walikuwa na ratiba ya kucheza mechi moja ya kirafiki uwanja wa Azam Complex, hata hivyo mpango huo hautakuwepo baada ya mapendekezo ya Kocha Miguel Gamondi
Gamondi hayuko tayari vijana wake wacheze mechi ikarushwa mbashara kabla ya Ngao ya Jamii kwani kufanya hivyo ni kuwaonyesha wapinzani wake silaha
Gamondi anataka kuwasurprise wapinzani wake kwa kuwashushia kikosi na mbinu ambazo hawakuzifahamu kabla
Hata Azam Fc ambao wana ratiba ya kuchuana na Bandari Fc Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex, awali mchezo huo ulitangazwa kuwa ungeonyeshwa mbashara na Azam TV, lakini kulingana na taarifa iliyotolewa na Azam Fc, hautaonyeshwa na pia mashabiki hawataruhusiwa
Yanga inatarajiwa kuelekea jijini Tanga siku ya Jumatatu tayari kuwakabili Azam Fc siku ya Jumatano
Post a Comment